Home Uncategorized AZAM FC YAFICHUA SIRI YA USHINDI MBELE YA WACONGO

AZAM FC YAFICHUA SIRI YA USHINDI MBELE YA WACONGO


ETTIENE Ndayiragije, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa haikuwa rahisi kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Kagame kutokana na ushindani walioupata ila jitihada ziliwabeba.

Azam imetinga  hatua ya fainali ya michuano ya Kagame baada ya ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya AS Maniema ya Congo baada ya kumaliza dakika 120 bila kufungana.

“Haikuwa rahisi kutinga hatua hii, kila timu ilikuwa inahitaji ushindi ila jitihada na mapenzi ya Mungu yametimia,” amesema.

Azam FC watacheza fainali hiyo dhidi ya KCCA ya Uganda kesho nchini Rwanda.

SOMA NA HII  SIMBA WAIJIBU KIBABE YANGA, NI KUHUSU SAINI YA BEKI CHIPUKIZI WA COASTAL UNION