Home Uncategorized BEKI MPYA MANCHESTER UNITED AMTAJA ALIYEMPELEKA UNITED

BEKI MPYA MANCHESTER UNITED AMTAJA ALIYEMPELEKA UNITED

AARON Wan- Bissaka ambaye ni beki mpya ndani ya Manchester United amesema kuwa meneja wa timu hiyo Ole Gunnar Solkjaer ndiye amesababisha ajiunge na timu hiyo.


Nyota huyo amejiunga na kikosi hicho akitokea Crystal Palace na ametambulishwa rasmi kuitumikia timu hiyo msimu ujao.

“Nimefurahi kutua Manchester United, wakati nikiwa kijana nilikuwa natamani sana siku moja nitue hapa na kocha Solskajaer ni mmoja wa watu waliosababisha mimi nikaja hapa,” amesema.
SOMA NA HII  BAADA YA KUPIGWA 5G,MAJIMAJI WATAJA ALIYEWAPONZA