Home Uncategorized DIDA: MANULA ALINIPA HASIRA YA KUPAMBANA

DIDA: MANULA ALINIPA HASIRA YA KUPAMBANA

DEOGRATIUS Munish ‘Dida’ amesema kuwa kuwekwa kwake benchi na mlinda mlango namba moja wa Simba Aish Manula kulimuongezea hasira ya kupambana.

Dida kwa sasa ameachana na Simba baada ya kumaliza kandarasi yake ya mwaka mmoja alikuwa anawekwa benchi muda mwingi na Manula wakati alipokuwa Simba.

“Kazi ya kumpanga nani aanze haikuwa mikononi mwangu, kocha ndiye aliyekuwa anaamua hivyo sikuwa na jinsi.

“Hali hiyo iliniongezea hasira na kunifanya nipambane kwa kufanya mazoezi na ndio maana kwenye mechi za mwisho nilipewa nafasi baada ya kocha kukubali uwezo wangu,” amesema Dida.

SOMA NA HII  MBELGIJI WA YANGA AOMBA MUDA KUKIJENGA KIKOSI KIWE BORA ZAIDI