Home Uncategorized KAKOLANYA: SIMBA WENYEWE WATANIPENDA

KAKOLANYA: SIMBA WENYEWE WATANIPENDA

BENO Kakolanya mlinda mlango mpya wa Simba ambaye amesaini kandarasi ya miaka miwili amesema kwamba hana mashaka na uwezo wake hivyo mashabiki watampenda.

Kakolanya amesema kuwa katika kazi kuna ulazima wa kupata changamoto mpya sina hofu na ushindani wa namba ndani ya Simba.

“Sina hofu na uwezo wangu na hata ndani ya Simba kwa kuwa najiamini na ninaweza kuleta ushindani, kuhusu namba mimi sina mashaka mwalimu ana chaguo lake nami kazi yangu ni kupambana kwa ajili ya timu yangu,” amesema.

Sasa Kakolanya atakuwa anagombania namba moja na mlinda mlango mwenye kandarasi ya miaka mitatu, Aish Manula. 

SOMA NA HII  GADIEL AWATUMIA UJUMBE WA KIBABE KENYA, WALA HANA HOFU