Home Uncategorized YANGA YAIPOTEZA SIMBA

YANGA YAIPOTEZA SIMBA

ZIMEBAKI siku tatu kuwakutanisha  Yanga na Simba Uwanja wa Taifa kwenye mechi nne za hivi karibuni ambazo ni dakika 360 Yanga imeipoteza Simba kwa kucheza mechi hizo bila kuruhusu bao.
Safu ya Yanga ya ulinzi inayoongozwa na Lamine Moro pamoja na Juma Abdul imeonyesha ukomavu kwa kuipoteza ile ya Simba inayoongozwa na Pascal Wawa sambamba na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.
Yanga imecheza mfululizo bila kuruhusu bao ilikuwa ni Februari 23 mbele ya Coastal Union 0-0, Februari 26,Gwambina FC 0-1 huu ulikuwa ni wa FA, Februari 29 Alliance 0-2 na Machi 3, Yanga 2-0 Mbao FC. Simba ndani mechi zao nne ambazo wamecheza mfululizo kabla ya mechi ya jana dhidi ya Azam FC walifungwa mabao 2 kwenye ushindi wa mabao 3-1, Februari 22, dhidi ya Biashara United, Februari 25 waliruhusu bao kwenye mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Stand United kwenye sare ya kufungana bao 1-1, ila walishinda kwa penalti 3-2 na kutinga hatua ya robo fainali.
Februari 18 haikufungwa mbele ya Kagera Sugar ikishinda bao 1-0 na Machi Mosi haikufungwa na KMC wakati ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Kwenye mechi hizo nne mfululizo Yanga imefunga mabao matano bila kuruhusu bao na Simba imefungwa mabao mawili na kufunga mabao sita.
SOMA NA HII  ISHU YA KUPIGWA FAINI NA BODI YA LIGI, UONGOZI YANGA WAJA NA TAMKO LINGINE LA KIBABE