KIKOSI cha Manispaa ya Kinondoni ‘KMC’ leo kimeripoti salama nchini Rwanda kwa ajili ya michuano ya kombe la Kagame.
Ofisa Habari wa KMC, Anwari Binde amesema kuwa wachezaji wamefika salama na wana morali nzuri kwa ajili ya kupambana kwenye michuano hiyo.
KMC ipo kundi A ambalo lina TP Mazembe ya Congo, Rayon Sports ya Rwanda na Atlabara ya Sudan Kusini.
Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Julai 7-21.