Home Uncategorized MASHABIKI WAITWA UWANJA WA TAIFA AGOSTI 28 KUIPA SAPOTI TIMU YA TAIFA

MASHABIKI WAITWA UWANJA WA TAIFA AGOSTI 28 KUIPA SAPOTI TIMU YA TAIFA

CLIFORD Ndimbo, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema kuwa ni wakati wa mashabiki kujitokeza kwa wingi Agosti 28 kuipa sapoti timu ya Taifa.

Taifa Stars itamenyana na Kenya Agosti 28 uwanja wa Taifa mchezo wa kufuzu michuano ya Chan uwanja wa Taifa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ndimbo amesema kuwa ni wakati wa Taifa kuungana kuipa sapoti timu ya Taifa.

“Timu ni yetu sote na tunapaswa kuipa sapoti kwa kujitokeza kwa wingi kuona namna timu itakavyopambana.

“Morali ni kubwa kwa kila mmoja na timu inaendelea salama kwa kufanya mzoezi uwanja wa Bocco na sasa wamehamia uwanja wa Taifa,” amesema.

SOMA NA HII  BARAKA MAJOGORO AZIINGIZA VITANI YANGA NA SIMBA