Home Uncategorized NAHODHA MPYA WA YANGA HUYU HAPA, ARITHI KITAMBAA CHA AJIBU

NAHODHA MPYA WA YANGA HUYU HAPA, ARITHI KITAMBAA CHA AJIBU

PAPPY Tshishimbi, kiungo wa Yanga amekabidhiwa kitambaa cha unahodha ndani ya kikosi hicho kilichoweka kambi mkoani Morogoro.

Kiungo huyo amekabidhiwa kitambaa hicho ambacho kilikuwa mikononi mwa Ibrahim Ajib ambaye amejiunga na Simba ambaye aliuchukua mikononi mwa Kelvin Yondani.

Kambi ya Yanga imeanza Julai 7 na bado inaendelea na kambi hiyo kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao na michuano ya kimataifa.

Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa wamekubalaina na uongozi kumpa kitambaa hicho kwa muda mpaka pale Zahera atakapowasili nchini.

SOMA NA HII  EXCLUSIVE: SIMBA YAMTANGAZA BENO KAKOLANYA