Home Uncategorized KABLA LIGI KUU BARA HAIJAANZA, RATIBA YA LIGI KUU BARA KUFANYIWA MABADILIKO

KABLA LIGI KUU BARA HAIJAANZA, RATIBA YA LIGI KUU BARA KUFANYIWA MABADILIKO

WILFRED Kidao, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa ratiba ya Ligi Kuu Bara msimu ujao ikafanyiwa marekebisho.

Kidao amesema kuwa mabadiliko hayo yanatokana na muingiliano wa mechi za kitaifa ambazo zitashirikisha timu nne msimu ujao.

“Haikuwa hesabu zetu kufanya hivi na hii inatokana na matarajio yetu ya timu ya Simba kuanza hatua ya awali kwani tulitarajia ingeanza kwenye hatua ya pili, kutokana na kutinga hatua ya robo fainali.

“Kwa sasa tunachokifanya ni kuangalia namna ya kuboresha ratiba yetu ili kuepuka viporo msimu ujao, kwa sasa tumeanza kufanyia kazi hivyo ni lazima tufanye jambo hilo kwani hata Afrika Kusni wao wamefuta kabisa ratiba kutokana na mambo kama haya,” amesema.

Timu nne za Bongo zinazoshiriki michuano ya kimataifa ni Simba na Yanga Ligi ya Mabingwa na Azam FC pamoja na KMC michuano ya kombe la Shirikisho.

Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 23 na mchezo wa ufunguzi utakuwa uwanja wa Taifa kati ya Simba na JKT Tanzania.

SOMA NA HII  PLAYOFF NGOMA NI NZITO, SASA MECHI ZA MWISHO KUAMUA