Home Uncategorized RUVU SHOOTING YAGOMEA WACHEZAJI WA KIGENI

RUVU SHOOTING YAGOMEA WACHEZAJI WA KIGENI


UONGOZI wa Ruvu Shooting umesema kuwa kwa sasa hauna mpango wa kusajili wachezaji kutoka nje ya nchi kutokana na kuamini uwezo wa wachezaji wa ndani.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa  klabu haina hesabu za kusajili nyota wa kigeni.

“Kwenye klabu yetu haitatokea tukasajili wachezaji wa kigeni, sura zao itakuwa ni ngumu kuonekana kwetu kwa kuwa tuna imani na wachezaji wa ndani.

“Kwa sasa tumeanza majaribio ya wachezaji wa ndani tukiwa na lengo la kusuka kikosi kipya hivyo tutawasili kwa kadri watakavyoonyesha uwezo wao,” amesema.

SOMA NA HII  LUC EYMAEL WA YANGA KUTUA BONGO JUNI 6