Home Uncategorized SIMBA: KWA USAJILI HUU NI MWENDO WA MAKOMBE TU

SIMBA: KWA USAJILI HUU NI MWENDO WA MAKOMBE TU


NYOTA mpya wa Simba, Ibrahim Ajibu amesema kuwa kwa namna kikosi kilivyo na kambi ya Afrika Kusini ilivyonoga lazima watetee kombe lao na kuleta ushindani kimataifa.

Simba imeweka kambi nchini Afrika Kusini ikiwa ni maalumu kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao imesajili nyota kadhaa wakali ikiwa ni pamoja na Gadiel Michael na Beno Kakolanya ambao walikuwa na Ajibu Yanga.

“Uhakika upo wa kutosha kwamba msimu ujao tutafanya makubwa na mengi, tunachohitaji ni kuona timu inabeba makombe mengi na kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa,” amesema.

Ajibu kwa msimu wa 2018-19 ni mchezaji aliyefanya vizuri kwenye ligi, ametoa assist 17 na alipachika mabao 6.

SOMA NA HII  VIDEO: USIPIME MAPOKEZI YA TUISILA NA TONOMBE WA YANGA