Home Uncategorized YANGA YATANGAZA MECHI NNE ZA MAAJABU

YANGA YATANGAZA MECHI NNE ZA MAAJABU


YANGA imetangaza kwamba mwezi Agosti na Septemba watakuwa na mechi nne za kuonyesha ubora wao Afrika lakini hapa kambini pamenoga. Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu itaanza Agosti 9, ingawa ratiba itatoka baada ya kumalizika kwa fainali za Afcon kesho Ijumaa.

Ndani ya miezi hiyo miwili, Yanga licha ya kwamba itakuwa ikicheza ligi ya ndani lakini italazimika kucheza mechi nne mbili za mtoano na mbili za raundi ya kwanza ili kusaka tiketi ya kufuzu hatua ya makundi. Mbili nyumbani na mbili ugenini.

Mwenyekiti wa Yanga, Dkt Mshindo Msolla amesisitiza kwamba lengo lao la kwanza ni kuhakikisha wanafi ka hatua hiyo ya makundi kwa kucheza kimahesabu mechi hizo nne.

Msolla ambaye ni msomi, alisema; “Kikubwa tulichokipanga ni kuhakikisha tunafi ka hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa Afrika.

Tulifanya usajili wa kisasa wenye wigo mkubwa wa wachezaji watakaocheza kwa kushindana na kutafuta kambi sehemu tulivu itakayomuwezesha kocha wetu Zahera kufanya kazi yake ya kuiandaa vizuri ambayo tuliipata ya Morogoro.”

Katika mazoezi ya jana jioni mjini hapa, walifanya wachezaji wachache huku wengine wakipumzishwa tayari kwa tizi zito la asubuhi. Jioni walifanya Metacha Mnata, Sadney Urikhob, Ally Sonso, Ally Ally, Balama Mapinduzi, Maybin Kalengo, Mrisho Ngassa, Fei Toto, Raphael Daud, Deus Kaseke na Said Makapu.

WIKI YA MWANACHI

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Dismas Ten alisema wiki yao iko palepale Agosti 4 na uwepo wa mechi ya Taifa Stars nchini Kenya hakuwezi kuwaathiri kwani wachezaji wao wengi wapo kikosini mjini hapa na mambo yanakwenda vizuri. Awali Yanga iliahirisha mechi hiyo dhidi ya AS Vita kupisha mechi ya Stars na Kenya Jijini Dar

SOMA NA HII  SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU KUREJEA LIGI