Home Uncategorized ARSENAL YAHAHA KUMPAMBANIA LACAZZETTE

ARSENAL YAHAHA KUMPAMBANIA LACAZZETTE


ALEXANDRE Lacazzette, mshambuliaji wa Arsenal kwa sasa anatibiwa majeraha yake aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya Lyon wikiendi iliyopita.

Lacazzette hakuwa sehemu ya kikosi kilichoivaa Barcelona kutokana na majeraha ya enka aliyonayo.

Anakabiliwa na kukimbizana na muda ambapo madaktari wanahaha kumrejesha kwenye ubora ili aanze kwenye mchezo wa ufunguzi dhidi ya Newcastle United Jumapili.

Nyota huyo mwenye miaka 28 ni miongoni mwa wapambanaji ambao wanaamiwa na Kocha Unai Emery.

Kwenye mchezo huo Arsenal mbele ya Barcleona ilipoteza kwa kipigo cha mabao 2-1.

SOMA NA HII  TUSIISAHAU PIA NA LIGI YA WANAWAKE KWA AJILI YA KUANDAA TIMU IMARA YA TAIFA