Home Uncategorized MKENYA AHUKUMIWA MAISHA, KOSA NI KUMBAKA MWANANAMKE MGONJWA ALIYE NA MIAKA 74

MKENYA AHUKUMIWA MAISHA, KOSA NI KUMBAKA MWANANAMKE MGONJWA ALIYE NA MIAKA 74


Raia wa Kenya, Anthony Mamboleo Nyakeo amehukumiwa kifungo hicho baada ya kupatikana na hatia ya kumdhalilisha kingono Mwanamke mgonjwa wa miaka 74

Nyakeo, aliyekuwa anafanya kazi kama Muuguzi Msaidizi katika Kituo cha Afya cha Woodrige kilichopo Grapevine anaelezwa kufanya kosa hilo mnamo Januari 2018

Mahakama ilielezwa Mtuhumiwa alifanya kitendo hicho kwa mgonjwa (Marehemu kwa sasa) aliyekuwa akiumwa ugonjwa wa kusahau (Alzheimer) huku akijua hawezi kujitetea

Baada ya kitendo hicho, Muuguzi anayemuhudumia mgonjwa alikuta damu kwenye nguo ya ndani na vipimo vilibaini uwepo wa michubuko ukeni inayotokana mara nyingi na kuingiliwa kwa nguvu

Mtuhumiwa huyo aliyebainika baada ya mgonjwa kufanyiwa kipimo vya vinasaba (DNA) alikana mashtaka kwa kusema vinasaba vyake vilipandikizwa kwenye mwili huo kutoka kwenye kondom aliyotumia

Hukumu hiyo inajiri ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu raia mwingine wa Kenya ahukumiwe huko Texas kwa kupatikana na hatia ya kuua Wanawake 11

SOMA NA HII  MOND, HARMONIZE WAKOSA TUZO ZA MVP 2020, WASHINDI HAWA HAPA