Home Uncategorized MTIBWA SUGAR: TUPO TAYARI KWA LIGI

MTIBWA SUGAR: TUPO TAYARI KWA LIGI


ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema maandalizi ya kikosi kwa ajili ya msimu mpya yanakwenda vizuri.

Mtibwa Sugar kibarua chake cha kwanza itakuwa ugenini dhidi ya Lipuli ya Iringa, Uwanja wa Samora, Agosti 25.

Akizungumza na Saleh Jembe, Katwila amesema kuwa imani kwa kikosi ni kubwa kutokana na maandalizi. 


“Imani ni kubwa kwa kikosi na maandalizi yanaendelea vizuri, wachezaji wana furaha na timu inapambana kuwa kwenye ubora wake muda wote. 

“Tupo sawa kwa sasa kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Bara, tuna imani ya kuleta ushindani ni suala la muda mashabiki watupe sapoti,’ amesema.

Mchezo wa kwanza wa Mtibwa Sugar utakuwa dhidi ya Lipuli ya Iringa utakaochezwa Uwanja wa Samora Agosti 25.

SOMA NA HII  AZAM FC KUKIWASHA LEO, MAJEMBE MAPYA KUTAMBULISHWA, KIBA ANA JAMBO LAKE