Home Uncategorized SIMBA KUILIPIA YANGA KIKAO NA WAANDISHI

SIMBA KUILIPIA YANGA KIKAO NA WAANDISHI


Na George Mganga,
Dar es Salaam

Uongozi wa Simba kupitia Ofisa Habari wake, Haji Manara, umesema utalipia gharama za kikao na waandishi wa habari ambacho wamedhamiria kukifanya kitakachohusisha wasema wa klabu zote zinazoshiriki mashindano ya kimataifa.

Tanzania Bara inawakilishwa na timu nne kunako michuano ya kimataifa ambazo ni Simba SC pamoja na Yanga zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa huku Azam FC na KMC FC zikishiriki Kombe la Shirikisho Africa.

Katika kikao na waandishi wa habari juzi, Manara alisema kuwa watafanya kikao hicho kwa ajili ya kuungana pamoja kuonesha utaifa sababu wote wanaiwakilisha nchi.

Alieleza kuwa wao kama Simba watahusika kugharamikia kikao hicho kwa kuwa wana uwezo wa kufanya hivyo.

“Tumepanga kufanya kikao cha pamoja na wasemaji wa timu zote zinazoshiriki mashindano ya kimataifa.

“Lengo letu kubwa ni kuonesha kwanza utaifa kwa kuwa tunaiwakilisha nchi, hakuna sababu ya kutofautiana, lazima tupeane sapoti.

“Sisi kama Simba tutagharamikia kikao hicho, hilo halitakuwa na shida sisi kwetu kama mabingwa wa nchi,” alisema Manara.


SOMA NA HII  KOCHA MPYA SIMBA ATOA MAAGIZO HAYA KWA MASTAA KABLA HAJATUA NCHINI