Home Uncategorized NYOTA MZAWA ANAYEWINDWA NA YANGA ATOA YA MOYONI

NYOTA MZAWA ANAYEWINDWA NA YANGA ATOA YA MOYONI

 


NYOTA wa JKT Tanzania Adam Adam ambaye ni mshambuliaji namba mbili kwa wazawa wenye mabao mengi amesema kuwa hawakuanza msimu vizuri jambo ambalo linawafanya wapambane kurejea kupata matokeo mazuri kwenye mechi zao zijazo.


Adam mwenye mabao sita ambaye jina lake linatajwa kuingia kwenye rada za mitaa ya Jangwani kwa kikosi cha Yanga kilicho chini ya Cedric Kaze anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat trick.


Alifunga hat trick hiyo na kusepa na mpira wake kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mwadui FC kwenye ushindi wa mabao 6-1 kisha nyota wa Simba, mshambuliaji bora wa muda wote, John Bocco akawa wa pili alipofunga wakati Simba ikishinda mabao 7-0 dhidi ya Coastal Union kwa msimu wa 2020/21.


Akizungumza na Saleh Jembe, Adam amesema kuwa msimu huu walianza vibaya kwenye mechi zao za mwanzo jambo lililowapotezea ramani ila wanaamini makosa watayafanyia kazi.


“Hatukuanza vizuri msimu huu ila bado tuna nafasi ya kufanya vizuri na kurejea kwenye reli, kikubwa ni mashabiki kuendelea kutupa sapoti nasi tutapambana kupata matokeo.


“Inaumiza kupata matokeo mabaya lakini hakuna namna kwa kuwa ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji matokeo chanya, nina amini makosa yetu benchi la ufundi litafanyia kazi,” amesema.


JKT Tanzania ipo nafasi ya 15 kwenye msimamo ikiwa imecheza mechi 11 imekusanya pointi 10 kibindoni.

SOMA NA HII  KUMBE ABDI BANDA ALIPOTEZA AMANI ALIPOHISIWA ANA CORONA