Home Uncategorized WAPINZANI WA LIVERPOOL LEO WAGOMA KUPAKI BASI

WAPINZANI WA LIVERPOOL LEO WAGOMA KUPAKI BASI


DANIEL Farke, bosi wa Norwich City leo amesema kuwa ana kazi ngumu leo mbele ya Liverpool kwenye mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu England mchezo utakaopigwa usiku.

Norwich watakuwa Uwanja wa Anflied kumenyana na Mabingwa wa Ligi ya Ulaya Liverpool.

Farke amesema kuwa hawana hofu mbele ya Liverpool licha ya ubora walionao kwa sasa ila watapambana kupata matokeo chanya.

Bosi huyo anewataka wachezaji wake wacheze Kwa kujiamini kwani uwezo wanao. 


“Tupo tofauti kwenye viwango vya ubora na wapinzani wetu ila tunapaswa tuonyeshe utofauti huo uwanjani hakuna sehemu nyingine. 

“Tutacheza Kwa tahadhari na hakutakuwa na mtindo wa kupaki basi, tunakuja tofauti msimu huu,”.

SOMA NA HII  KOCHA MPYA LIPULI ABEBA MATUMAINI MAPYA