Home Uncategorized YANGA: MASHABIKI JITOKEZENI TAIFA MUONE BURUDANI

YANGA: MASHABIKI JITOKEZENI TAIFA MUONE BURUDANI

MSHINDO Msolla, Mwenyekti wa Yanga amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi siku ya Agosti 4 uwanja wa Taifa kuona namna watakavyotoa burudani.

Agosti 4 uwanja wa Taifa itakuwa ni kilele cha siku ya Mwanachi ambapo Yanga itamenyana na Kariobangi Shark kutoka Kenya.

Msolla amesema:”Kikosi kimejipanga kufanya vizuri na tunaamini ushindani utakuwa mkubwa kwani wapinzani wetu sio wa kubeza ukizingatia kwamba walifanya vizuri kwenye michuano ya SportPesa pamoja na kushinda mbele ya Everton.

“Mashabiki wasisahau kununua pia na jezi pamoja na vifaa halisi ambavyo vinapatikana makao makuu ya Yanga pamoja na maduka ya GSM, ile hofu ya kuwa hatutapata faida waiondoe, na kazi iwe moja kuiunga mkono timu” amesema.

SOMA NA HII  MISRI YATUPWA NJE AFCON KWA KUCHAPWA BAO 1-0 NA AFRIKA KUSINI, LORCH APELEKA MSIBA