Home Uncategorized YANGA SASA KULA SAHANI MOJA NA WABOTSWANA, WATUA BONGO KIBABE

YANGA SASA KULA SAHANI MOJA NA WABOTSWANA, WATUA BONGO KIBABE


YANGA leo imerejea kutoka visiwani Zanzibar ambapo waliweka kambi maalumu kujiandaa na mchezo wao wa kimataifa dhidi ya Township Rollers utakaochezwa kesho uwanja wa Taifa.

Yanga itamenyana na Township Rollers ya Botswana majira ya saa 12:00 uwanja wa Taifa ukiwa ni mchezo wa awali wa kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa. 

Mchezo wa pili wa marudio unatarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 23-25 nchini Botswana.

Mrisho Ngassa amesema kuwa wapo tayari kwa ushindani na imani yao ni kupata matokeo chanya mbele ya wapinzani wao.

SOMA NA HII  C7 MUGALU WA SIMBA ATAKIWA KUFUNGA MABAO MENGI