Aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Yanga, Ahmed Amasha, leo ametembelea makao makuu ya klabu hiyo na kutoa zawadi ya vifaa mbalimbali vya soka.
Amasha ametoa vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi za kitanzania milioni 3.
Vifaa hvyo ni mipira, koni, beeps na vinginevyo.
Mchango huo umetolewa na Amasha kwa ajili ya kuongeza morali ya wachezaji kuelekea maandalizi ya msimu ujao wa ligi na michuano ya soka Afrika.