Home Uncategorized ZAHERA ATUMA UJUMBE KWA MASHABIKI YANGA

ZAHERA ATUMA UJUMBE KWA MASHABIKI YANGA


MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ameandaa dozi maalum kwa ajili ya Ruvu Shooting mchezo utakaochezwa leo Uwanja wa Uhuru.

Zahera alisema kuwa amewaambia wachezaji wake wote kuwa mchezo wa kwanza ni muhimu kwao kushinda.

“Tunaanza rasmi ligi kwa kucheza na Ruvu Shooting siyo timu ya kubeza kwa kuwa ipo ndani ya ligi, nimewaambia wachezaji wangu ni lazima tuwape dozi maalum wapinzani wetu kujiweka kwenye mazingira bora msimu huu.

“Tuna kazi ngumu kimataifa hilo lipo wazi lakini ndani ya ligi pia ni muhimu na niliwaambia awali kwamba tunakuja kupambana kutwaa taji la ligi na safari ndiyo inaanza kwa sasa,” alisema Zahera.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, alisema kuwa kikosi kipo salama na wanachohitaji ni pointi tatu muhimu.

SOMA NA HII  KUMBE ULIMWENGU ALIZICHOMOLEA SIMBA, YANGA ISHU IKO HIVI