MBWANA Samatta, nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ amesema kuwa anawashukuru mashabiki wa Tanzania kwa kutoa sapoti kubwa jana wakati timu ikimenyana na Burundi jambo linalowapa matumaini ya kufanya makubwa Septemba nane uwanja wa Taifa.
Stars jana ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na timu ya Burundi kwenye mchezo wa kwanza wa kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.
Samatta amesema :”Tumeona namna ambavyo nguvu ya mashabiki imetupa nguvu ya kufanya makubwa na kupambana kwa ajili ya Taifa mwisho wa siku tumeambulia sare ya ugenini.
“Kwetu sio matokeo mabaya tunamaini tutafanya vema wakati mwingine ukizingatia kwamba tutakuwa nyumbani na tuna amini itakuwa kazi moja kutafuta ushindi,” amesema.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.