Imeelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Yanga bado haujawalipa fedha wachezaji wake ambazo ni shilingi milioni 50 za kitanzania.
Yanga waliahidiwa fedha hizo baada ya kuitupa nje Township Rollers katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mabao 2-1.
Taarifa zinaeleza kuwa wachezaji hao hawajajua mpaka sasa uongozi umekwama wapi juu ya fedha hizo walizoahidi.
Fedha hizo ziliahidiwa kuwa zitakuwa sehemu ya motisha kwa wachezaji hao ili wazidi kufanya vema katika michuano ya kimataifa.
Hivi sasa Yanga ipo katika maandalizi kuelekea mechi ya hatua ya kwanza dhidi ya Zesco United ya Zambia.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.