Home Uncategorized SIMBA KUSHUSHA STRAIKA MKALI ZAIDI YA OKWI, NI HUYU HAPA

SIMBA KUSHUSHA STRAIKA MKALI ZAIDI YA OKWI, NI HUYU HAPA


Inaelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Simba upo kwenye mipango ya kushusha straika wa maana katika dirisha dogo la usajili.


Maamuzi hayo yanakuja kutokana na safu ya ushambuliaji wa Simba kuonekana na mapengo kadhaa tangu kuondoka kwa Mganda, Emmanuel Okwi.

Taarifa za ndani kutoka Simba zinasema uongozi unajipanga hivi sasa kuhakikisha anakuja straika wa maana atakayezidi kiwango cha Okwi kwa ajili ya kuongeza makali.

Straika huyo atakuwa ni wa kimataifa na bado haijajulika nchi atakayotokea maana bado haijawekwa wazi.

Inaelezwa lengo kubwa la kuhitaji straika mwingine ni namna Simba walivyokosa umakini katika mechi na UD Songo ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika ufungaji wa mabo.
SOMA NA HII  SVEN AMTEGA SHEVA MSIMBAZI