Home Uncategorized NGORONGORO HEROES YAANZA KWA USHINDI SAUDI ARABIA

NGORONGORO HEROES YAANZA KWA USHINDI SAUDI ARABIA

 


JAMHURI Khiwelo, wengi wanapenda kumuita Julio jana Desemba 11 alikiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka  20, Ngorongoro Heroes kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Saudi Arabia.


Mchezo huo wa kirafiki ulichezwa Uwanja wa Prince Saud Bin Jalawi ulikuwa ni wa kwanza kwa Ngorongoro Heroes ambayo imeweka kambi nchini humo kwa ajili ya maandalizi ya Afcon pamoja na mashindano mengine.


Ikiwa imeweka kambi kwenye Mji wa Al Khoba ulio Mashariki mwa Saudi Arabia, jana ulikuwa  ni mchezo wa kwanza kwa kuwa walitumia siku mbili kuwa chini ya uangalizi kutokana na sheria ya Saudi Arabia katika kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.


Bao pekee la ushindi lilifungwa na mzawa Ben Starkie baada ya kipa kutema mpira uliokuwa  unakwenda nyavuni.


Julio amesema kuwa waliwazidi wapinzani wao katika mbinu licha ya kuonyesha ushindani ndani ya dakika 90 kwenye mchezo huo.

SOMA NA HII  BEN CHILWELL APIGA HESABU ZA KUSEPA LEICESTER CITY