Home Uncategorized MANCHESTER DABI LEO,GUARDIOLA HATUA KWA HATUA NA OLE

MANCHESTER DABI LEO,GUARDIOLA HATUA KWA HATUA NA OLE

 


PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester City amesema kuwa hatua kwa hatua leo atapambana na Manchester United inayonolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer.


Leo Desemba 12, Uwanja wa Old Trafford,  Manchester United itamenyana na Manchester City ikiwa ni Manchester Dabi itakayokuwa na ushindani mkubwa majira ya saa 2:30 usiku.


Rekodi zinaonyesha kuwa timu hizi zimekutana mara 182 na leo inakuwa ni mara ya 183 tangu zianze kukutana na mara ya kwanza ilikuwa ni Novemba 12,1881.


Manchester United imeshinda  jumla ya mechi 76 na City imeshinda jumla ya mechi 54 na zimekusanywa jumla ya sare 52 na utakuwa ni wa 47 tangu Premier League ibadilishe mfumo mwaka 1992.

SOMA NA HII  NAFASI YA HAJI MANARA SIMBA YAGOMBEWA KWA KASI YA KUTISHA