Home Uncategorized WACHEZAJI 10 WENYE THAMANI KUBWA ZAIDI DUNIANI KWA SASA

WACHEZAJI 10 WENYE THAMANI KUBWA ZAIDI DUNIANI KWA SASA


Shirika linalojihusisha na utafiti wa mikatba ya wachezaji na thamani zao katika soko la usajili na hadhi za timu la CIES Football observatory, umetoa listi ya wachezaji wenye thamani kubwa zaidi katika soko barani Ulaya.

Utafiti wa CIES umemulika zaidi kwa wachezaji wanaocheza  katika ligi kubwa tano bora barani ulaya yaani ligi za England, Hispania, Ujerumani, Italia, na Ufaransa, ambapo thamani za wachezaji hawa zimekadiliwa kwa kuzingatia umri, klabu anayochezea, nafasi anayocheza, ligi anayocheza, urefu wa mkataba katika klabu yake, taifa analotokea lakini pia ni anahitajika na timu za aina gani katika soko la usajili.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya PSG Kylian Mbappe ametajwa kuwa mchezaji mwenye thamani zaidi barani ulaya akifuatuiiwa na Raheem Sterling wa Manchester city na  na Mohamed Salah wa Liverpool.

Mbappe mwenye miaka 21 ametajwa kuwa na thamani ya pesa za Uingereza pauni million 225, huku Raheem Sterling wa Manchester city na timu ya taifa ya England akishika nafasi ya pili akiwa na thamani ya pauni million 190 nafasi ya tatu ni Mohamed Salah raia wa Misri anaekipiga katika klabu ya Liverpool ya England ametejwa kuwa na tahamani ya pauni million 149.

Mchezaji bora wa Dunia mara 6, Lionel Messi ametejwa kuwa na thamani ya pauni million 107 akiwa katika nafasi ya  8 miongozi mwa wachezaji wenye thamani zaidi katika ligi kubwa tano barani ulaya wakati Cristiano Ronaldo hayupo katika orodha hiyo yenye jumla ya wachezaji 20.

Hii ni orodha ya wachezaji 10 wenye thamani barani ulaya kwa mujibu wa CIES Football observatory, kwa viwango vya pesa ya Uingereza: 1. Kylian Mbappe (£225m), 2. Raheem Sterling (£190m), 3. Mohamed Salah (£149m), 4. Jadon Sancho (£143m), 5.  Sadio Mane (£132m), 6.  Harry Kane (£128m), 7. Marcus Rashford (£114m), 8.  Lionel Messi (£107m), 9. Antoine Griezmann (£105m), 10. Lautaro Martinez (£98m.
SOMA NA HII  SIMBA NA YANGA YAPIGANA VIKUMBU KUPATA SAINI ZA MITAMBO HII YA MABAO