Home Uncategorized NYOTA WA KMC AFICHUA KILICHO NYUMA YA MAFANIKIO YA KUTEMBEZA MABAO 5-0...

NYOTA WA KMC AFICHUA KILICHO NYUMA YA MAFANIKIO YA KUTEMBEZA MABAO 5-0 MBELE YA PAN AFRICAN


CHARLSE Ilanfya, mshambuliaji wa KMC amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa kurejea Uwanjani kutokana na kusmbuliwa na majeraha kwa muda mrefu,

Ilanfya alijiunga na KMC kwenye usajili wa dirisha dogo, alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya misuli aliyoyapata msimu wa 2018/19 wakati timu yake ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Jana alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda mabao 5-0 wanja wa Uhuru dhidi ya Pan African kwenye mchezo wa hatua ya 32 bora ya kombe la Shirikisho a inasonga mpaka hatua ya 16 bora.

Bao lake lilikuwa la mwisho alifunga dakika ya 778 na wa kwanza kufunga alikuwa ni James Msuva dk ya 12, Serge dk 22 na mawili yalifungwa na Sadala Lipangile dk 45 na 73.

“Namshukuru Mungu kwa kunipa nguvu na nimerejea Uwanjani, kwangu ni furaha kurejea kwenye kazi ninayoipenda mashabiki waendelee kutupa sapoti,” amesema.

SOMA NA HII  YANGA: NTIBANZONKIZA ATAFUNGA MABAO MENGI