Home Uncategorized MASHABIKI WAOMBWA KUIPA SAPOTI LIPULI, LIGI NI MOTO

MASHABIKI WAOMBWA KUIPA SAPOTI LIPULI, LIGI NI MOTO


PAUL Nonga nahodha wa Lipuli amesema kuwa ligi ya msimu huu wa 2019/20 ni ngumu jambo linalowafanya wapambane wakiwa ndani ya uwanja kupata matokeo.

Lipuli ipo nafasi ya nane ikiwa na pointi zake 25 baada ya kucheza mechi 17 imefunga jumla ya mabao 25 ambapo Nonga amehusika kwenye jumla ya mabao 12 akifunga nane na kutoa jumla ya pasi nne za mabao.

“Ligi ya msimu huu imekaza na kila timu inapambana kupata matokeo jambo hilo linatufanya nasi tupambane kupata matokea chanya, mashabiki waendelee kutupa sapoti,” amesema Nonga.

SOMA NA HII  KIUNGO POLISI TANZANIA ATUMA UJUMBE KWA WATANZANIA WOTE KUOMBEANA DUA