Home Uncategorized MORRISON, MASHINE MPYA YA YANGA YAZUNGUMZIA ISHU YA USHINDANI WA NAMBA

MORRISON, MASHINE MPYA YA YANGA YAZUNGUMZIA ISHU YA USHINDANI WA NAMBA


KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison amesema kuwa kilichomtoa Ghana mpaka Bongo ni kazi tu jambo ambalo linamfanya afikirie kufanya vema muda wote.

Morrison amesajiliwa na Yanga kwenye dirisha dogo msimu huu na tayari ameonyesha makeke yake kwenye mchezo dhidi ya Singida United wakati timu yake ikishinda kwa mabao 3-1 Uwanja wa Namfua.

Nyota huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya mbili uwanjani amesema kuwa :”Ninatambua kitu kilichonileta ndani ya Yanga, sina hofu na ushindani wa namba kwa kuwa nimecheza timu kubwa jambo linalonipa hali ya kujiamini,” amesema.

 Yanga ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa imecheza jumla ya mechi 15 ina pointi 28 kibindoni.

SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU BARA HUU HAPA