ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa kilichoifanya timu yake kushindwa kupata matokeo mbele ya Tanzania Prisons ni ubovu wa Uwanja wa jamhuri ambao waliutumia.
Mtibwa Sugar iliambulia pointi moja mbele ya Tanzania Prisons na walipata pigo la kumkosa kiungo wao Abdulhalim Humud ambaye alionyeshwa kadi nyekudu.
“Nashukuru kupata pointi moja ugenini, haikwuwa malengo yetu na tumeshindwa kutokana na mazingira ya uwanja kutokuwa rafiki kwetu kupata matokeo.
“Nawapongeza wachezaji kwa kujituma, makosa ambayo yametokea tutayafanyia kazi ili kurejea kwenye ubora wetu kwenye mechi zinazofuata,” amesema.
Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 24 imecheza mechi 23 za ligi.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.