Home Uncategorized GREALISH MSHIKAJI WA SAMATTA ANAWINDWA NA MANCHESTER UNITED

GREALISH MSHIKAJI WA SAMATTA ANAWINDWA NA MANCHESTER UNITED


JACK Grealish, mchezaji nyota wa timu ya Aston Villa amewekwa kwenye rada za Manchester United pamoja na Leicester City ambao wanahitaji kuipata saini yake.
Nyota huyo ambaye anakipiga timu moja na Mbwana Samatta, raia wa Tanzania amekuwa akifuatiliwa kwa ukaribu na klabu nyingi kutokana na ubora wake akiwa ndani ya Uwanja.
Ameisaidia timu yake kutinga hatua ya Fainali ya Kombe la Carabao Cup msimu huu na amehusika kwenye jumla ya mabao tisa na kutoa jumla ya pasi tano za mabao.
Rekodi za Grealish zimezivutia timu nyingi ambazo zimeanza kumvutia kasi ili kupata huduma ya nyota huyo kwenye timu zao ikiwa ni pamoja na Tottenham .
Nyota huyo mwenye miaka 24 amekuwa msaada mkubwa ndani ya timu hiyo iliyo chini ya Dean Smith ikiwa inahaha kubaki ndani ya Ligi Kuu England, ipo nafasi ya 17 imecheza mechi 25 na ina pointi 25.
SOMA NA HII  HUYU HAPA KOCHA BORA WA MWEZI JANUARI, MZUNGU WA SIMBA NA MALALE HAMSINI WAPIGWA KIKUMBO