Home Habar za Usajili Simba KISA OFA NONO KUTOKA ORLANDO PIRATES… ONYANGO AGOMEA MKATABA MPYA WA SIMBA..ISHU...

KISA OFA NONO KUTOKA ORLANDO PIRATES… ONYANGO AGOMEA MKATABA MPYA WA SIMBA..ISHU IKO HIVI..


Klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini imeripotiwa kutaka huduma ya beki wa Klabu ya Simba Joash Onyango anayemaliza mkataba wake na Simba mwishoni mwa msimu huu.

Tayari Onyango amepewa Ofa ya kwanza na Klabu ya Simba ya kusaini mkataba mpya lakini Onyango ameipiga chini ofa hiyo akitaka kuboreshewa zaidi maslahi yake.

Onyango ndio beki tegemeo wa Simba kwa sasa akiwa anacheza sambamba na Henock Inonga Baka, Alijiunga na timu hiyo misimu miwili iliyopita akitokea Gor mahia ya nchini kwao Kenya.

Wakati anasajiliwa na Simba wakati huo, alitoka kushinda tuzo la mchezaji mwenye thamani zaidi nchni Kenya.

SOMA NA HII  PABLO AKAZIA ISHU YA SIMBA KUWA NA KIPORO KISA MECHI NA WASAUZI...AMWAGA 'DATA' HADHARANI...