Home Uncategorized KOCHA SIMBA AELEZA KINACHOMSUMBUA KUHUSIANA NA SAFU YA USHAMBULIAJI

KOCHA SIMBA AELEZA KINACHOMSUMBUA KUHUSIANA NA SAFU YA USHAMBULIAJI


SVEN Vanderbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa bado anasumbuliwa na tatizo la safu ya ushambuliaji kushindwa kumalizia nafasi wanazotengeneza pamoja na safu ya ulinzi kushndwa kulinda lango.

Simba ambao ni mabingwa watetezi wa ligi, jana Februari,4 walishinda mabao 2-1 mbele ya Polisi Tanzania ya Moshi ambao walianza kwa kasi kipindi cha kwanza na kufunga bao lao pekee dakika ya 22 kupitia kwa Sixtus Sabilo aliyefunga mtaa akiwa na mabeki wawili Haruna Shamte na Keneddy Juma.

Kwa upande wa Simba, John Bocco aliweka mzani sawa dakika ya 56 kabla ya Ibrahim Ajibu kufunga bao la ushindi dakika ya 90.

Sven amesema: “Kuna tatizo ambalo lipo na nimeliona kwenye mechi zangu zilizopita na hii pia nimeliona, nitazungumza na wachezaji wangu kuona namna gani tutalimaliza tatizo hili,”.

Simba imecheza jumla ya mechi 19 ipo kileleni ikiwa na jumla ya pointi 50, imepoteza mchezo mmoja mbele ya Mwadui FC  kwa kuchapwa bao 1-0 na ilitoa sare mbili mbele ya Yanga kwa kufungana mabao 2-2 na Tanzania Prisons ya bila kufungana.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUMCHAKAZA WILDER KWA TKO, FURRY ALIKUWA AMEONGOZA RAUNDI ZOTE SABA KWA POINTI