Home Uncategorized MBARAKA YUSUPH AREJEA RASMI AZAM FC BAADA YA KUWA NJE MWAKA MMOJA

MBARAKA YUSUPH AREJEA RASMI AZAM FC BAADA YA KUWA NJE MWAKA MMOJA


MBARAKA Yusuph, mshambuliaji wa Azam FC amerejea uwanjani baada ya kukaa nje kwa muda wa mwaka mmoja.

Mbaraka alikuwa anasumbuliwa na majeraha ya goti aliyoyapata wakati akiitumikia timu ya Namungo ambayo imepanda Daraja kwa sasa inashiriki Ligi Kuu Bara.

Habari kutoka Uongozi wa Azam FC zinaeleza kuwa Mbaraka alianza mazoezi rasmi jana, Februari 9, Jumapili na wachezaji wenzake wa Azam FC.

Yusuph alifanyiwa upasuaji wa goti lake la mguu wa kulia Aprili mwaka jana katika Hospitali ya Vincent Pallotti jijini Cape Town, Afrika Kusini, kufuatia kubainika kuchanika mtulinga wa kati wa goti hilo (Anterior Cruciate Ligament Tear).

SOMA NA HII  KOCHA MKUU WA SIMBA ATUA NCHINI LEO