Home Uncategorized MBEYA CITY SASA KICHEKO WAREJEA SOKOINE, KUANZA KAZI NA LIPULI LEO

MBEYA CITY SASA KICHEKO WAREJEA SOKOINE, KUANZA KAZI NA LIPULI LEO

MBEYA City leo wataikaribisha Lipuli kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Sokoine.

Huu utakuwa mchezo wa kwanza kwa timu hizi msimu huu kutumia Uwanja huo wa Sokoine baada ya kuzuiwa na Bodi ya Ligi kwa muda wa mwezi mmoja, kutokana na sehemu yake ya kuchezea kuharibika kutokana na kufanyika tamasha katika sehemu ya kuchezea.

Lipuli ilipoteza mchezo wake uliopita kwa kufungwa bao 1-0 itamenyana na Mbeya City ambayo imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Ruvu Shooting.

Kocha wa Mbeya City Amri Said amesema kurejea ndani ya Uwanja wa nyumbani kwao ni faraja kwa wachezaji na mashabiki watafurahi kuona timu imerejea nyumbani.

SOMA NA HII  NAMUNGO WATUSUA KIMATAIFA,NGOMA UGENINI YAWA 3-3