Home Uncategorized MZUNGU AMBADILISHIA MAJUKUMU NCHIMBI KISA MOLINGA

MZUNGU AMBADILISHIA MAJUKUMU NCHIMBI KISA MOLINGA


LUC Eymael amesema kuwa kazi kubwa aliyompa mshambuliaji wake Ditram Nchimbi ni kutengeneza nafasi za mabao kwa mshambuliaji mwenzake David Molinga akishindwa basi inabidi afunge yeye mwenyewe.
Pacha ya Nchimbi na Molinga imeonekana kujibu ambapo kwenye mechi mbili wameipa pointi sita timu yao kwa kuhusika kwenye mabao mawili ya ushindi.
Mchezo wa kwanza mbele ya Mtibwa Sugar, Nchimbi alimtengenezea pasi Molinga aliyefunga bao lake la sita kwa kichwa Uwanja wa Taifa na kwenye mchezo wa juzi Uwanja wa Uhuru Nchimbi alimtengenezea pasi ya bao Molinga mbele ya Ruvu Shooting na Yanga ilishinda bao 1-0.
Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa miongoni mwa vitu ambavyo anavifanyia kazi kwa ukaribu ni uwezo wa safu ya ushambuliaji kufunga na kutengeneza mabao jambo linalomfanya ambadilishie majukumu Nchimbi.
“Nchimbi naona ana kitu kizuri mguuni mwake na jicho lake limekuwa karibu na Molinga ndio maana nimekuwa nikimtaka awe anaanzia pembeni lakini haina maana kwamba hapaswi kufunga nalo ni jukumu lake pia ndani ya uwanja.
“Molinga yeye asili yake ni moja hatulii uwanjani kazi yake kuzunguka hili pia ni tatizo lingine ila kinachonifurahisha anajua kukaa kwenye nafasi na kufunga hapo tu siangalii staili za kufunga kikubwa ni pointi tatu na nina amini watakuwa na mwendelezo mzuri,” amesema.
Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 37 mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Mbeya City, Februari 11,2020, Uwanja wa Taifa, saa 1:00 usiku.
SOMA NA HII  WACHEKA NA NYAVU NDANI YA LIGI KUU ENGLAND HAWA HAPA