Home Uncategorized WACHEZAJI WAMPA NGUVU KOCHA NAMUNGO

WACHEZAJI WAMPA NGUVU KOCHA NAMUNGO


HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo amesema kuwa anakoshwa na uwezo wa wachezaji wake ndani ya uwanja jambo linalompa hali ya kujiamini.

Thiery amekiongoza kikosi chake kuwa ndani ya 10 bora baada ya kucheza mechi 21 na kinashika nafasi ya sita kibindoni kina pointi 37.

“Wachezaji wanacheza kwa kujituma ndani ya uwanja kitu pekee ambacho kinatufanya tupate matokeo ambayo tunahitaji ndani ya ligi.

“Ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji ushindi kama ilivyo kwetu, mashabiki waendelee kutupa sapoti,” amesema.

SOMA NA HII  MKATABA WALIOSAINI YANGA,GSM NA LA LIGA UPO NAMNA HII