Uncategorized

USHNDI WA MABAO 2-0 MBELE YA NDANDA YAIPA JEURI MTIBWA SUGAR

admin March 2, 2020 1:19 pm

OFISA Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa kwa sasa klabu hiyo imerejea kwenye ubora baada ya kushinda mabao 2-0 mbele ya Ndanda mchezo uliochezwa Uwanja wa Gairo, Februari 29.

Mabao ya Mtibwa Sugar yalifungwa na Juma Liuzio dakika ya 11 kwa pasi ya Riphat Khamis na bao la pili lilifungwa na Haruna Chanongo dakika ya 85.

Kifaru amesema: “Hatukuwa kwenye mwendo mzuri hasa kwenye mechi zetu saba za nyuma kwa kuwa tumeanza kushinda tunarejea kwenye kasi yetu na mambo mazuri yanakuja mashabiki watupe sapoti.

“Wakata miwa kwa sasa tumezinduka na tutaendeleza vita ya kusaka pointi tatu kwenye mechi zetu zote,” amesema.

Mechi inayofuata kwa Mtibwa Sugar itakuwa Jumatano, Uwanja wa Gairo dhidi ya Namungo FC ya Lindi.

CR 7 KUMBE AMEHUSIKA KICHAPO CHA BARCELONA YA MESSI MBELE YA REAL MADRID CIOABA KWENYE MTIHANI MZITO MNDANI YA BONGO, JUMATANO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply