Home Uncategorized GUARDIOLA; HAIKUWA RAHISI KUTWAA TAJI LA CARABAO MBELE YA ASTON VILLA YA...

GUARDIOLA; HAIKUWA RAHISI KUTWAA TAJI LA CARABAO MBELE YA ASTON VILLA YA SAMATTA



PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester Ciy amesema kuwa haikuwa kazi nyepesi kushinda ubingwa mbele ya Aston Villa kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Carabao iliyopigwa Machi Mosi, Uwanja wa Wembley.
City ilitwaa ubingwa huo mbele ya Villa anayokipiga nyota wa Tanzania, Mbwana Samatta baada kutumia dakika 20 kupata bao la kuongoza kupitia kwa Sergio Arguero.
Bao la ushindi la City lilifungwa na Rodri Hernandez alipachika bao  la pili na la ushindi dakika ya 30 na kuifanya Villa kupambana kutafuta ushindi ili kutwaa taji hilo licha ya kukwama.
Samatta alipachika bao la kwanza kwenye fainali hiyo kwa timu yake ya Villa dakika ya 41 kwa pasi ya Anwar El Ghazi na kuipa matumaini Villa kupindua meza mambo yakawa magumu.
Bao hilo la kichwa lilimchanganya Guardiola kwani alionekana akishangaashangaa kwa namna kichwa cha Samatta kilivyonasa mpira ule na amesema kuwa haikuwa rahisi kwao kutwaa ubingwa.
SOMA NA HII  SIMBA:MECHI YETU DHIDI YA AZAM FC NI YA KISASI