Home Uncategorized HASIRA ZA SIMBA KUPIGWA NA YANGA ZAHAMISHIWA SINGIDA UNITED, YAICHAPA 8-0

HASIRA ZA SIMBA KUPIGWA NA YANGA ZAHAMISHIWA SINGIDA UNITED, YAICHAPA 8-0


KIKOSI cha Simba leo kimeibuka na ushindi wa mabao 8-0 mble ya Singida United kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Simba iliingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa bao 1-0 na Yanga huku Sinigida United ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa bao 2-1 na Tanzania Prisons jambo lililofanya timu zote zcheze kwa kukamiana.

Meddie Kagere alifunga mabao manne kwenye mchezo wa leo ambapo alifungua pazia dakika ya 1 kwa pasi ya Tshabalala, dk 25  baada ya kukutana na mpira uliotemwa na kipa dk ya 41 na dk 71 kwa pasi ya Dilunga.

Mengine mawili yalifungwa na Deo Kanda dk 12 kwa pasi ya Kapombe,na dk ya 18 pasi Bocco, John Bocco alifunga bao moja dk ya 19 na Sharaf Shiboub alifunga bao moja dk 59 kwa pasi ya Deo Kanda.

Singida United ilimaliza ikiwa pungufu baada ya mchezaji wao Haruna Moshi ‘Boban’ kuonyeshwa kadi nyekundu dk 52 kwa kumpiga kiwiko Manula.


Ushindi huo unaifanya Simba kuwa nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 71 baada ya kucheza mechi 28 huku Singida United ikiwa nafasi ya 20 baada ya kucheza mechi 28 na ina pointi 12.

SOMA NA HII  BEKI WA YANGA MWAMNYETO AMFUNIKA MAGUIRE WA MANCHESTER UNITED