Home Uncategorized KADI YA NJANO ALIYOPEWA ,MATTEO WA ARSENAL YAZUA BALAA HUKO, MASHABIKI WAMVAA...

KADI YA NJANO ALIYOPEWA ,MATTEO WA ARSENAL YAZUA BALAA HUKO, MASHABIKI WAMVAA REFA


KADI ya njano aliyoonyeshwa mchezaji wa Arsenal, Matteo Guendouzi na refa Mike Dean imezua balaa kwa mashabiki wakidai kwamba ni kadi ya ajabu kutokea.

Guendouzi alionyeshwa kadi hiyo kwenye mchezo wa Kombe la FA England mbele ya Portsmouth iliposhinda mabao 2-0 kwa kitendo chake cha kutumia nguvu nyingi kuweka chini mpira ili apige mpira wa adhabu.

Kupitia kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii baadhi ya mashabiki ikiwa ni pamoja na Dan Critchlow ameandika kuwa kadi ya njano ya Mike Dean hajawahi kuiona ikitokea ndo mara yake ya kwanza.

JBTM ambaye ni shabiki wa Arsenal amesema kuwa Mike Dean ni shabiki wa Spurs.


Dean amesema kuwa anafanya kazi kwa kuzingatia kanuni na utaratibu kwani amekuwa refa kwa muda wa miaka 10.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA YANGA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA JAMHURI, KOMBE LA MAPINDUZI