Home Uncategorized NAKUKUMBUSHA WAZIRI LUKUVI, MIUNDOMBINU IELEKEE KWA KINA SAMATTA WAPYA

NAKUKUMBUSHA WAZIRI LUKUVI, MIUNDOMBINU IELEKEE KWA KINA SAMATTA WAPYA





NA SALEH ALLY
HIVI karibuni Serikali Ya tanzania imeeleza namna ambavyo imefanya vizuri katika kutatua migogoro ya ardhi ikionekana ni kipindi ambacho mwafaka umepatikana kuliko wakati mwingine wowote.


Utatuzi wa migogoro ni jambo muhimu sana, kwa maana ya asili wanadamu wakikaa pamoja, lazima kutakuwa na kutofautiana, kuwe kwa asili au makusudi.


Katika suala la ardhi kweli kumekuwa na migogoro mingi sana na kama imepatiwa mwafaka kwa kuwa mingi imekuwa ikiendana na dhuluma. Basi Serikali inapaswa kupongezwa sana sana.


Wakati tunaipongeza Serikali kuhusiana na migogoro hiyo, naona ni wakati mzuri sana pia wa kuikumbusha Serikali kuhusiana na suala la miundombinu inayojali suala la sehemu maalum ambazo zitakuwa zinatumika kwa ajili ya michezo.


Sehemu maalum Kwa ajili ya michezo ambazo zitasaidia kuzaliwa kwa wanamichezo wengine kwa ajili ya wakati ujao kwa kuwa tunaona kuna kila sababu ya kufanya namna hiyio.


Tunastahili kufanya hivyo kwa kuwa sasa tuna kila sababu ya kusema tumejithibitishia mara nyingi zaidi kwamba michezo si stared pekee badala yake ni agira na biashara kubwa.


Ukiangalia katika michezo mingi, utaona mwanzo ilionekana ni burudani tu, sasa mambo yamebadilika na tunaanza kuamini kile ambacho waandishi tumekuwa tukikisema bila ya mafanikio.


Vijana wetu sasa wanapata ajira, ndani na nje ya Tanzania na wengine wanalipwa mishahara mikubwa kuliko madaktari na walimu au maprofesa wa vyuo vikuu na hii ndivyo ilivyo dunia nzima.


Kama hitoshi, michezo hii inalipa kodo kubwa. Mfano, angalia mechi ya Yanga na Simba kwa siku moja inaingiza zaidi ya Sh milioni 500 lakini kwa siku hiyo wafanyabiashara kibao wanaouza vitu kama maji, nguo na kadhalika wanafaidika kwa kiasi kikubwa.


Michezo ina faida kubwa na hii ndio maana yangu kwamba huu ni wakati mzuri sasa Serikali kuacha kuichukulia michezo kama sehemu ya burudani tu au kisiasa.

Mfano kunapokuwa na michezo basi viongozi wa Serikali au vyama vya siasa watafika pale na kuzungumza maneno matamu na kuondoka zao. Watasubiri tena hadi watakapoalikwa kuwa wageni rasmi waaksere maneno matamu yanayokwenda na upepo na hakuna chochote kinachofanyika kuisaidia michezo.


Shukrani kwa Rais John Magufuli, yeye alikumbuka hata kuomba uwanja kutoka kwa Seirkali ya Morocco na tunatarajia siku moja atakumbukwa kwa uwanja huu ambao ninaamini utaibadilisha Dodoma.


Ushauri sasa ni kwa Waziri wa Ardhi, William Lukuvi. Kwa kuwa mwendo wake umekuwa mzuri na anapambana vilivyo na wanaovunja sheria za ardhi na kusababisha migogoro zikiwemo zile dhuluma za wazi. Huu ni wakati mzuri wa kuhakikisha mipango miji wanaangalia suala la sehemu za wazi kwa ajili ya michezo.


Wadogo na watoto zetu wanastahili kupata sehemu za wazi. Mfumo wa milano miji yetu kumekuwa na tatizo kubwa sana la sehemu za wazi. Watu wanaona sehemu kubaki wazi ni kama haara. Kama unakumbuka waziri mmoja wakati wa uongozi wa Rais Jakaya Kikwete eti alitaka pale UWanja wa Nyamagana ijengwe hoteli kwa kuwa sehemu inatumika kwa hasara na uwanja huwa haukai mjini. Niliwahi kumshauri atembelee Camp Nou, Barcelona au Santiago Bernabeu, Madrid akajifunze.


Ukiangalia sehemu karibu zote zile ambazo kwa sasa zimeanza kujengeka katika jiji la Dar es Salaam, huoni sehemu za wazi kwa ajili ya watoto ambao ninaamini wakikua katika mazingira ya kimichezo, pamojana afya njema lakini tunaweza kuzalisha wanamichezo bora kabisa.


Hili litiliwe mkazo, hili lisiwe la hadithi na tusiangalie leo tu badala yake Waziri Lukuvi lishikilie kwa ajili ya kizazi kijacho.

SOMA NA HII  DUBE ATAJA KINACHOWAPA UGUMU NDANI YA LIGI KUU BARA