Home Uncategorized NAMUNGO: TULIWAHESHIMU YANGA

NAMUNGO: TULIWAHESHIMU YANGA

BIGIRIMANA Blaise, mshambuliaji wa Namungo FC amesema kuwa walingia uwanjani wakiwaheshimu Yanga jambo lililowapa hali ya kujiamini na kuweza kugawana nao pointi mojamoja kwa kufungana bao 1-1.

Mabao yote ya jana yalifungwa kwa mtindo wa vichwa ambapo walianza Yanga dakika ya sita kupitia kwa Tariq Seif akimalizia pasi ya Juma Abdul na Namungo walifuata dakika ya 62.

Blaise amesema kuwa haikuwa kazi nyepesi kupata bao mbele ya Yanga kutokana na uimara wa kikosi cha wapinzani wao.

“Yanga ni timu kubwa na ina wachezaji wazuri, tuliingia uwanjani kucheza nao kwa kupambana na kila mchezaji alikuwa na majukumu yake, kwa sasa tunasema asante kwa kuwa tumepata pointi moja sio mbaya,” amesema.

Namungo kwenye Uwanja wa Majaliwa imecheza mechi 14 na imepoteza mechi moja ikilazimisha sare nne na imeshinda mechi 9.
SOMA NA HII  KIKOSI CHA TAIFA STARS KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA DR CONGO