Home Uncategorized NIYONZIMA ACHEKELEA MAISHA YAKE NDANI YA YANGA

NIYONZIMA ACHEKELEA MAISHA YAKE NDANI YA YANGA

HARUNA Niyonzima, kiungo mshambuliaji ndani ya Yanga amesema kuwa kwa sasa anafurahia maisha ndani ya klabu hiyo kutokana na sapoti anayopata kutoka kwa wachezaji wenzake.

Akizungumza na Saleh Jembe, Niyonzima amesema kuwa kila sehemu kuna changamoto zake lakini maisha yake ndani ya Yanga yanampa furaha.

“Nipo ndani ya Yanga kwa sasa maisha yanaendelea na kila mmoja anafurahi maisha ya mwenzake ndivyo ilivyo kwa sasa na ninaendelea kufurahi kuwa hapa.

“Mashabiki wamekuwa nasi bega kwa bega tukiwa ndani ya Dar hata wakati ule tulipokuwa tukitoka nje ya Dar, ni kitu kizuri kwetu pia,”amesema Niyonzima.

Niyonzima alikipiga pia Simba msimu uliopita wa 2018/19 alisepa baada ya mkataba wake kuisha na kuibukia AS Kigali ya Rwanda kwa sasa anakipiga ndani ya Yanga.

SOMA NA HII  EXCLUSIVE:MORRISON ASIMULIA ALIVYOCHOMWA SINDANO NNE KUIMALIZA SIMBA