UONGOZI wa klabu ya Yanga umekataa kuwa haukumtuhumu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makondo kuhusu jambo lolote linalohusiana na Yanga.
Taarifa hiyo imekuja kutokana na kusambaa kwa taarifa zisizo rasmi kwenye mitandao ya jamii kwamba alisema Yanga haikuwa na uwezo wa kuifunga Simba huku ikieleza kuwa barua iliyosambazwa ilikuwa ni ya watu ambao si wa kutoka katika ofisi za kalbu hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Yanga, David Ruhango imeeleza kuwa Yanga haihusiki kwa namna yoyote na taarifa zinazoenea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu tuhuma za Klabu ya Yanga kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar.
Mchezo wa pili wa Ligi Kuu Bara Yanga iliwanyoosha Simba kwa bao 1-0 Uwanja wa Taifa.