OLE Gunnar Solskajer, Kocha Mkuu wa Manchester United amewataka wachezaji kutumia muda huu wa mapumziko kupata ushauri kutoka kwa wapenzi wao, wake zao ili kupata nguvu ya kufanya mazoezi.
Ligi Kuu England pamoja na ligi nyingine duniani zimezimamishwa kutokana na kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.
Solskajer amesema:” Katika wakati huu mgumu ambao tunapitia itakuwa vema kwa kila mchezaji kutumia ushauri wa mke wake ama mpenzi wake ili kupata nguvu ya kufanya mazoezi.
“Muhimu kwa wachezaji kufanya hili jambo ili kulinda vipaji vyao na inawezekana kwao kuwa bora,” amesema.