Uncategorized

ILIKUWA KITAMBO, SAINI YA NAHODHA WA MTIBWA SUGAR NA SASA NI KOCHA MKUU, CHEKI MAFANIKIO YAKE

admin April 13, 2020 12:27 pm

KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila mkataba wake wa kwanza kusaini ilikuwa ni mwaka 1999 mbele ya mmoja wa wakurugenzi wa wakati huo Mr. Bube.

Katwila alikuwa kwenye wakati mzuri alipojiunga na Mtibwa Sugar kwani mwaka huo wa 1999 timu yake ilitwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara na ilitetea pia taji hilo mwaka 2000 kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru.

Pia Katwila akiwa ni nahodha alikiongoza kikosi hicho kutwaa Kombe la Mapinduzi mwaka 2000 na alikuja kukiongoza tena kikosi hicho kutwaa Kombe la Mapinduzi mwaka 2020 kwa kuitungua Simba bao 1-0.

Katwila amesema:”Nakumbuka nilitwaa taji la Mapinduzi nikiwa nahodha mwaka 2000, ilikuwa ni wakati mzuri kwetu na timu kiujumla,”.

ISHU YA CHAMA NA KANDA YANGA WAIKOMALIA, HUYU HAPA SAUTI YA MWISHO POLISI TANZANIA YATUMA UJUMBE HUU KUHUSU VIRUSI VYA CORONA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply