AMISS Tambwe ni nyota wa zamani wa Yanga na Simba alicheza ndani ya Ligi Kuu Bara kwa mafanikio makubwa na kuweza kushika chati ndani ya Yanga pia hata alipokuwa Simba.
Emmanuel Okwi raia wa Uganda anayekipiga pia kwenye timu ya Taifa pia ni nyota wa zamani wa Simba na Yanga alicheza kwa mafanikio makubwa alipokuwa Bongo kwenye Ligi Kuu Bara.
Wote hawa wawili ni washambuliaji na wakati mwingine walikuwa wanaweza kucheza wakiwa viungo ila kwa kutegemea mwalimu anatumia mfumo gani.
Hawa ni wachezaji wa kigeni ambao kwa namna moja ama nyingine walikuwa wanalichangamsha soka la Bongo pale wanapokuwa uwanjani.
Hii inatokana na namna ambavyo wanaweza kukupa matokeo wakati usiotarajia na kukufanya uamini kwamba mpira upo kwenye damu zao.
Kwa sasa nyota hao wote hawapo Bongo wanaendelea na maisha yao nje huku mmoja ambaye ni Okwi anakipiga nchini Misri na mwingine akiwa zake maskani Burundi huyo ni Tambwe.
Okwi yeye ni raia wa Uganda ambapo wakati anaondoka alikuwa ndani ya Simba ilikuwa msimu wa 2018/19 na alitwaaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara pia alitupia mabao 15.
Kwa Tambwe yeye wakati akiwa Yanga 2018/19 alikutana jumla na janga la kuachwa mazima huku ikielezwa kuwa amechuja ila alitupia mabao nane ndani ya ligi.
Hapo ndipo ambapo huwa ninaufurahia usajili wa Bongo ni wa sarakasi kibao na timu ikishamchoka mtu basi habari zinakuwa nyingi.
Hebu tujadili kidogo hapa baada ya Tambwe kusepa waliomfuata walifanya nini cha ziada ndani ya Yanga ambayo ilifanya usajili matata?
Aliletwa David Molinga raia wa Congo akaletwa Juma Balinya wa Uganda hao tu wawili ngoja nikuongezee mmoja anaitwa Patrick Sibomana nini wanachojivunia kwa sasa?
Hapo Molinga ambaye ni namba moja kwa utupiaji mabao hana nafasi kikosi cha kwanza, Sibomana pia ana mabao matano huyo Balinya hesabu zake ziloshafungwa kwani alishachimbishwa.
Sasa hapo ndipo huwa pananichanganya yaani yule anayeachwa anaonekana ni bora kuliko yule aliyepo ndani hii ni mbaya kwa timu zetu katika hili ni janga.
Molinga ana mabao nane kwa sasa ikiwa ni mfungaji namba moja ndani ya Yanga hii ni nzuri lakini ana nafasi gani uwanjani.
Ngoja turudi kwa Okwi huyu mbadala wake ilielezwa alikuwa ni mbarazil Wilker da Silva hatma yake ameishia kucheza dakika tatu ndani ya Ligi Kuu Bara kisha akapigwa chini hili ni tatizo inabidi lifanyiwe kazi.
Suala la kusajili wachezaji linahitaji umakini na sio kufanya kwa kuwa mwenzano anafanya ninaamini kwamba iwapo Simba ingechanga karata zake vizuri bila papara ingepata washambuliaji wazuri ama ingekubali kubaki na Okwi kisha mshahara wa kuwapa Wabrazil angebeba Okwi.
Yote kwa yote ni sehemu ya maisha kwamba ikifika wakati wa usajili wengi wanapenda kushindan maisha ya soka hayapo hivyo yanahitaji umakini na kuchanga karata vizuri.